Ujue umuhimu wa zawadi katika penzi!!!!

Status

HABARI za mda huu vijana wenzangu,karibuni sana katika pande hizi za vijana na mahusiano ili tuweze kuhabarishana habari nyingi zinazohusu mahusiano na maisha yetu ya kimahusaiano kama vijana ili tuweze kuboresha mapenzi yetu na kudumu kwa mda mrefu katka uchumba na ndoa zetu.
Leo katika mada yetu tunazungumzia juu ya habari ya zawadi katika penzi na jinsi gani zawadi inavyoweza kuboresha na kustawisha penzi lenu.Katika hii dunia wakati wa ujana ndio wakati wakutafuta mwenzi utakaye jumuika naye katika maisha yakte hadi kifo kitakapowatenganisha.Kama tunavyojua hakuna raha hapa duniani kama kupendwa na na wewe kuonesha thamani ya mpenzio lazima umpende kwa dhati kwa matendo mbalimbali ili naye afurahie mahusiano mliyonayo.
Kijana lazima utambue jinsi ya kulilinda na kulitunza penzi la akupendaye,na njia mojawapo ya kulitunza penzi ni ZAWADI.Ninapoongelea zawadi namaanisha ya aina yoyote ile ambayo unahisi itamfanya mwenzi wako ahisi na kutambua pendo lake kwako.Unaweza ukanunua ua,kadi yenye maneno mazuri ya mahaba,viatu,gauni au kitu chochote kile ambacho kitakuwa kumbukumbu nzuri kwa mwezi wako,hata kama anapanga kukusaliti,akiangalia zawadi ile ama kuikumbuka basi lazima nafsi itamsuta na kujikuta akiacha kukusaliti na kubaki akikuwaza wewe.
Jifunze jinsi ya kuuteka moyo wa mwenzi wako kwa kumnunulia zawadi .Maana unakuta watu wengine wako katika mahusiano au ndoa kwa mda wa miaka mitatu nakuendelea ,kwao hawajui hata zawadi ni nini kwa mwenzi wake zawadi yake anawza fedha na mapenzi tu.mjali mpenzi wako kwa zawadi japo mara moja kwa mwezi au hata kununulia kitu mabacho amekimiss na anakipenda zaidi hapo lazima utamfurahisha sana kwani hata kama ukimpa pesa zitaisha lakini zawadi ataikumbuka daima.
Ijenge akili yako iamii kuwa zawdi ni kitu muhimu sana kuliboresha penzi la mwenzi wako ,kwani zawadi hushawishi na kusababisha akuamini kuwa unampenda,na pia zawadi huweka kumbukumbu nzuri ndani ya akili na kamwe kumbukumbu ya zawadi haifutiki mapema kama ilivyo kumbukumbu ya pesa,maana waliompapeasa ni wengi lakini uliyemnunulia shati na perfume ni wewe.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s